|
SIRI
imefichukua kuwa madai kwamba ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul Jumaa
‘Diamond Platnumz’ ni memba wa jamii ya siri inayodaiwa kumwabudu shetani,
Freemason a.k.a Wajenzi Huru zilianza kitambo lakini sasa zimeshika kasi baada
ya kunaswa kwa picha inayomuonesha akisalimiana na
mtasha kwa ishara ya Kifreemason.
Picha ya tukio hilo
lilijiri nchini Uingereza, mwaka jana Diamond alipokwenda kwa ajili ya kufanya tamasha.
Inasadikiwa kwamba mavazi anayotumia mwanamuziki huyo kuwa ni
meusi, yalifanana sawia na yale ya
mtasha, yanayoelezwa kuwa sehemu ya mavazi yanayotumiwa na jamii ya Freemason.
Ishara nyingine ya salamu ya wawili hao ambayo ilitengeneza
nembo ya Freemason ya bikari kwa namna walivyogusanisha vidole vyao.
Wadau waliyoiona picha hiyo kupitiamtandao wa kijamii wa Twitter, wanasema kwamba Diamond amekuwa na
ishara nyingine nyingi za aina hiyo hali inayopelekea kuzua utata na kuamini
kwamba ni memba wa jamii hiyo ya Siri.
|
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi