Saturday, June 16, 2012

Jide ala Birthday bila Gadner G Habash

Mwanamuziki nguli wa muziki wa kizazi kipya Judith Wambura jana Juni 15 alikuwa akisherekea siku ya kuzaliwa kwake, wakati huo Mc wa sherehe hiyo alikuwa Elias Barnaba 'Barnaba Boy au Barnaba Classic', ambaye pia aliungana na mwanamuziki huyo katika kutupa vipande vya nyimbo zake ikiwemo ile ya Njia panda ambayo iliamsha watu kwenye viti. Jide alifanya sherehe hiyo wakati mumewe Gadner G Habash hakuwepo, lakini hata hivyo sherehe ilienda vizuri ingawa watu wengi walitaka kujua nini kilijili, maana si kawaida na waliotegemea huenda likatolewa taarifa yoyote ya kutokuwepo kwake lakini jambo ambalo halikufanyika. Sherehe ya kuzaliwa kwake iliudhuliwa na wasanii mbali mbali ikiwemo wa muziki wa kizazi kipya watangazaji pamoja na wanamuziki wa taarabu.
Jide akikata keki kwaajili ya kuwalisha walioudhulia
Jide akilishwa keki
Keki ina mambo, yaani hata kama analishwa mwenzako lazima na wewe ufumbue mdomo... Hivi uliwahi kujiuliza kwa nini.
Huyu alikuwa kwa niamba ya mashabiki.
Baada ya hapo burudani ilikuwa kama kawaida, Jide na bendi ya machozi
Utunzaji kama kawaida ulichukuwa nafasi yake

Jide alipendeza sana pia alipiga vibao vile vya zamani na sasa
Hapo ndipo utakapojua mziki wetu unapendwa hao aupendi, hadi wazungu walikuja kujumuika ndani ya Nyumbani Loudge
Barnaba aliwashika vizuri na kibao cha njia panda, Magubegube na vingine vikali kama hivyo.

Rechal wa Bongo Movie, naye ndani ya mduara
Mama wa Taarabu Khadija Omari Kopa, akijadili na mumewe Kharifan juu ya kwenda kujitupa uwanjani.
Ukiwa mwanamuziki unakuwa kama mafuta ya petroli yanapoona moto, akamwacha mumewe akajumuika kati ya kuyarudi yale yale.
Jack Patric ndani ya nyumba
Mc Barnaba Boy, anasema yeye siku hiyo hakusimama kama mwanamuziki Barnaba, eti alikuwa kama Mc


Yote tisa kumi ikabaki kwa huyu,kilammoja alikuwa akijiuliza ni mwanamke au mwanamme,jambo ambalo hakuna aliyepata jibu mpaka watu wanaondoka mjengoni.
Hapa akiyarudi mduaraa
Hakuwa nyuma sana katikakucheza.
Kila penye jambo hapakosi mambo, kazi kwenu

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi