|
NYOTA wa filamu nchini Steven Nyerere kesho saa 6 mchana anatarajia kutoa shukrani zake
kwa watoto yatima na kusali misa fupi katika kanisa la Ananasifu katika
kutimiza ahadi aliyoiweka katika uzinduzi wa filamu yake ya Mr Presedent.
Stive alisema kufanya hivyo ni kuonyesha shukrani zake kutokana
na kwenda vizuri kwa filamu yake, na aliahidi kwamba lazima atoe japo sadaka
kidogo kwa watoto waishio mazingira
magumu.
Alisema pia ameshaachia filamu yake mpya ya Respect Nyerere,
ambayo anaamini nayo itafanya vizuri kama ilivyokuwa kwa Mr Presedent.
“Kazi zangu zitaendelea kuwa za kuhamasisha na kutoa
mafunzo zaidi na sio za mapenzi kama
wengine wanavyofanya” alisema.
|
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi