TULIJADILI
HILI-TUMESHAMPUMZISHA NDUGU YETU KATIKA NYUMBA YAKE YA
MILELE...MUNGU AMREHEMU!! But kuna mengi yamekuwa yakizungumzwa...
1. Kitendo cha mh. Rais kuhudhuria....msibani...pale nyumbani Sinza!!watu wanamlaumu mh.rais kwamba...wamefariki viongozi wengi wakubwa
kama wakuu wa mikoa,wabunge,wakuu wa majeshi lakini hakuhudhuria akatuma
mwakilishi, lakini kwa kanumba amekwenda!! Watu wanazidi
kufunguka kuwa kwa kwenda kwa rais haoni kama ametumia nguvu kubwa ya
ulinzi kumlinda pale pamoja na viongozi wengine, ambayo ni gharama
kubwa!!why asingetuma mwakilishi tu! Je kanumba ni special kuliko mkuu wa
mkoa au mbunge? pia ikalaumiwa pia eti kwanini serikali inapoteza pesa
kupanga matrafiki,askari wengi ktk msiba huu, mwingine akasema gharama za
mafuta ya ile helicopter au zile mil kumi za J.K aliyotoa km
rambirambi eti angezipeleka tu kwa watoto yatima!! sio yakasemwa mengi
sana! lakini mie naamini rais hajafanya kosa...ktk marais wote wa Tz
waliopita ikumbukwe huyu ndo' rais aliye karibu sana na sanaa, na ana
mapenzi na wasanii, so amefanya yale kwa upendo mkubwa...kwasababu kanumba
alitangaza bendera yetu nje ya nchi pengine hata pasipo suport ya
serikali!! So kwa hili mimi simlaumu mh.rais...ww unaonaje? 2. Lakini
jingine ni kuhusu APPRECIATION...nimekuwa nikiliongelea sana hili, kuwa
wabongo hatuna kawaida ya kukubaliana sisi kwa sisi...marehemu kanumba mara
kwa mara tulikuwa tunakutana nae, maisha club,Leaders club,coco beach, kwenye
live band,maofisini,hata barabarani, lakini tulikuwa tukimpotezea tu
pengine hata salamu hatukuwa tunampa....hata movie zake wengine
walidiriki kuziponda, aah hawezi huyo movie itakuwa bongo?movie ni 24 na
prison break bn! Wengi hatukuwa watu wa kumpa mawazo chanya bali
kumponda na kumdiscourage!! lakini jamaa hakukata tamaa alikuwa anajua
anachofanya!! ...so enzi za uhai wake...wengi sio wote hatukuwa watu wa
kumkubali kama inavyoonekana hapa!! Najiweka miongoni mwao ili kuleta
attention ya hiki ninachoandka!! lakini tazama leo alipofariki ule umati
wote unalia,unaomboleza kwa majonzi, unaonyesha wote wanamkubali WHY?
|