Kampuni ya
Bi Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kiliminjaro Prenium Lager kwa
kushirikiana na baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) leo wametangaza rasmi tarehe
ya usiku wa kutoa Tuzo za Muziki Tanzania (Kilimanjaro Tanzania Music Award)
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es salaam,Meneja wa bia ya Kilimanjari Bwana
George Kavishe alisema tarehe ya siku ya kutoa tuzo hizo ni tarehe 12 april
2012 ndani ya ukumbi wa Mlimani City.
“Shughuli
itaanza rasmi saa moja jioni ikipambwa na burudani safi ilipangwa kwa umahili
na mtaalam kutoka nyumbani. Wanaii watao panda usiku wa kutoa tuzo ni pamoja na
Diamond, kundi zima la Tmk Wanaume, Charles Baba, Kharid Chokoraa, Recho, Ommy
Dimpozi, Bichuka na wengine” alisema Kavishe.
Aliendelea
kusema, tamasha litakuwa kali kwani sio tu waitaimba nyimbo zao lakini wataimba
na nyimbo za zamani zilizowahikutamba za kwao pamoja na wanamuziki nguli
nchini.
Pia meneja
wa Kilimanjaro ametoa shukrani kwa Watanzania
kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kupiga kura .
“Tumevuka
lengola idadi ya kura kwa Nyanja zote ni maana ya ujumbe mfupi wa simu,
vipeperushi, barua pepe na mitandao hii imaanisha Tuzo za zimekubalika na
zimepokelea na jamii”
Aidha
aliendeleakutoa shukrani kwa BASATA kwa kuendelea kutoaushirikiano na bia ya Kilimanjaro
na kuipatia tena kibali cha kudhamini na kuendeleza shughuli za Tuzo za Muziki Tanzania.
Tiketi
zitauzwa kwa kwa VIP shilingi elfu 75 ikijumuishwa na chakula cha jioni
(Buffet) na vinywaji bulena kawaida kwa shilingi elfu 20, na bia moja ya bule.
Tiketi
zitauzwa maeneo ya Ukumbi wa Mlimani City kuanzia jumatatu, Posta
Mpya ‘Baraka Golden mtaa wa Azikiwe nyuma ya CRDB Bank’, Zizzou Fashion ya Victoria, Sinza na
Tegeta, Bornie To Shine Mwenge, Robby One Fashen Kinondoni, Engine Petrol
station Mbezi.
mwisho
|