Thursday, March 15, 2012

Sasa tifu tifu la Bongo Fleva lawaka ndani kwa ndani

Wasanii wa Bongo Fleva ambao wanaunda kundi la Bongo Fleva Unity 'BFU' ambalokiongozi wake ni Mwana Fa na Saidi Fella huku likikusanya wasanii karibu wote ambao wanaimba muziki wa Bongo Fleva,kama hapo juu mnavyowaona katika timumoja, pamoja na wasanii wa Chama cha wasanii Tanzania 'TUMA' bado wapo kwenye ushindani mkali wa majadiliano baada ya wasanii ambao wengi wao waliunda kundi la Anti Virus kutaka ya nyuma si ndwele tugange ya yajayo kwa kuombana radhi. Lakini wasanii wa BFU wamedai kwamba hakuna kuombana radhi kwakuwa wao hawajawatukana wasanii hao, ila wao ndiyo waliotukananwa na kudhalilishwa.
Hali hiyo ilipelekea kukosekana kwa maelewano mbele ya waziri wa Michezo Nchimbi pamoja na msuhishaji wake Erick Shigongo, ambao ndiyo waliofanikiwa kuwasuruhisha kati ya Mbunge wa Mbeya Sugu na Luge. Wasanii wa BFU wanadai kwamba hakieleweki mpaka waombe radhi, lakini wasanii wa  TUMA  wanadai wasamehane na sio kuombana radhi, chezo hilolilipelekea kutoka bila ya maelewano na kikao kughairishwa mpakakeshompaka suluhu itakapopatikana. Mchezo bado wa moto ndani kwa ndaniiiiiii

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi